Sababu halisi za Depression
"Nilikuwa na miaka 18 tu nilipomeza kidonge changu cha kwanza cha antidepressant." Haya ni maneno ya mwandishi Johann Hari, akielezea wakati alipoamua kutafuta msaada wa kitaalamu kutokana na kuzorota kwa afya yake ya akili. Akiwa anapambana na tatizo la unyogovu, alimueleza daktari wake hali yake. Daktari, kwa kumuelezea kwa ujasiri, alimwambia, "Unyogovu ni ugonjwa wa ubongo. Kuna tatizo katika ubongo wako ndiyo maana unajisikia hivi. Dawa hii itakusaidia kurekebisha tatizo hilo."
#Unyongofu kwa lugha nyingine ni depression
Daktari alimwambia Hari, "Kuna watu ambao kiasili wana viwango vidogo vya serotonini, na hii ndiyo sababu huwa wanapata unyogovu na kukosa furaha."
Cha kushangaza, daktari hakumuuliza maswali yoyote kuhusu maisha yake. Hakutaka kujua kama kuna mambo yoyote yaliyokuwa yanamsumbua au kama kuna chochote kilichokuwa kinamchangia kuhisi vibaya. Badala yake, alichagua kumwandikia dawa, na kwa miaka 13 iliyofuata, Johann Hari aliendelea kutumia dawa hizo, huku dozi ikiongezwa mara kwa mara. Alitarajia kuwa kadiri dozi inavyoongezeka, ndivyo angeanza kuhisi vizuri, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya. Kwa miaka mingi, huzuni iliendelea kumlemea, bila kujali ukubwa wa dozi aliyokuwa anatumia.
Hii ndiyo story nyepesi sana ambayo imekuwa ikitawala mjadala kuhusu matatizo ya afya ya akili, hasa unyogovu: kwamba ni tatizo la kibiolojia linalotokana na hitilafu katika ubongo, na suluhisho lake ni rahisi sana - dawa.
Lakini, swali linabaki: kwa nini watu wanaendelea kuwa na unyogovu hata wanapotumia dawa? Na kwa nini, mwaka baada ya mwaka, viwango vya unyogovu vinaendelea kuongezeka?
Depression ni tatizo sugu ambalo linaathiri takriban watu milioni230 duniani kote Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO):Viwango vya depression vinazidi kuongezeka kila kukicha je sababu ni ile ambayo daktari alimuelezea Johann hari hapo juu? na kama sababu ni hiyo je ni shida katika ubongo wa mtu au kuna mengine mengi ambayo bado hatujayatambua ?
Ni swali ambalo alijiuliza Johann na lilimfanya kuanza kutafuta sababu halisi zinazosababisha depression na baada ya mahojiano na wataalamu wengi wa afya ya akili kuzunguka maeneo mengi duniani aliweza kuja na vile ambavyo ameviandika kuwa ni sababu halisi za depression
kama ifuatavyo
1.Cause One: Disconnection from Meaningful Work
Je unaifanya kazi yenye maana? Johann Hari ameweka wazi kwamba watu wanapotengwanishwa na kazi yenye maana wapo hatarini zaidi kupatwa na depression alionyesha moja ya utafiti uliowahi kufanyika
Kati ya mwaka 2011 na 2012, kampuni ya upigaji kura ya Gallup ilifanya utafiti wa kina zaidi kuwahi kufanywa kuhusu jinsi watu ulimwenguni kote wanavyohisi kuhusu kazi zao. Walisoma mamilioni ya wafanyakazi katika nchi 142. Waligundua kuwa asilimia 13 ya watu wanasema wana shauku na wamejitolea kwa kazi zao na wanachangia shirika lao kwa njia chanya.
Kinyume chao, asilimia 63 wanasema hawana shauku na kazi wanayofanya
Na asilimia nyingine 24 ni sio tu kwamba hawajishuhulishi kazini hawa hawafurahi kazini kwa asilimia kubwa watu wengi unakuta hawapendi kazi wanazozifanya na matokeo yake ni kwamba inakuwa rahisi zaidi wao kuwa na huzuni nyingi msongo mkali zaidi wa mawazo na depression
Kama sehemu ambapo unatumia zaidi ya asilimia 70 ya maisha yako panakupa stress na huzuni unategemea nini?
Bila shaka ni moja kati ya mengi yanayoendelea kuongeza janga la depression
2.Cause Two: Disconnection from Other People
Upweke na depression ni kama marafiki wapendanao hawa mara nyingi utawakuta pamoja na uhusiano wao unashangaza kidogo watu wenye depression hali wanayopitia huwavuta na kuwaweka katika upweke mkali ,hivyo hivyo watu wapweke nao wana hatari kubwa zaidi ya kupata depression
Upweke unazidi kuongezeka limekuwa tatizo kali kiasi kwamba baadhi ya nchi kama Uingereza januari mwaka 2018 waliweka rasmi utaratibu wa kuwepo kwa waziri wa upweke nchi zingine kama Japan pia zimefuata utaratibu huo mpaka sasa umeona namna ambavyo tatizo limezidi kuwa kali na linazidi kuongezeka kila kukicha
katika kitabu hiki mwandishi alirejea kazi ya miongoni mwa watu wa kwanza walioanza kusoma kuhusu athari za upweke alirejea kazi ya Prof John Caccioppo ameweka wazi kwamba mahusiano ya karibu kazi yake sio kutufurahisha ila kutufanya tujihisi kuwa tupo salama
3. Disconnection from Meaningful Values
Kila mmoja wetu "mpaka sasa una uelewa namna ambavyo kuna kitu hakipo sawa na aina ya vyakula vinavyotumika sana siku hizi na vinagharimu afya zetu taratibu nilipokuwa najifunza kuhusu "depression na anxienty" najifunza kwamba kuna jambo pia linatokea katika maadili (values) ambazo zinatufanya tuumwe kihisia" ni maneno ya mwandishi
Values ni nini?Ni yale mambo yanayoongoza matendo na maamuzi ya mtu kujua kinachofaa na kisichofaa na yanaathiri mtazamo au hata motisha ya mtu na utu pia
mwandishi anaelezea kwamba alipokuwa kijana mdogo ilionekana kwamba furaha ilikuja kwa kununua vitu vingi na kuvionyesha
katika safari yake ya kujifunza kuhusu depression alijifunza kwamba kama values za mtu zipo sana kuhusu namna ambavyo watu wengine wanamuona mtu huyo hatakuwa na furaha na mwisho wa siku ataishia kwenye depression hizo ndizo ambazo aliziita junk values
hata ukiangalia katika jamii viwango vya kile ambacho kinaitwa materialism kinazidi kuongezeka
tafiti zinaonyesha kwamba tangu janga la KORONA viwango vya materialistic values ambazo kwa kiasi kikubwa zinahamasisha upweke zimeongezeka zaidi
soma zaidi utafiti huo hapa
Je KORONA imeongeza materialism?
Cause Four: Disconnection from Childhood Trauma
Hapa mwandishi alieleza wazi namna ambavyo childhood trauma inavyoweza kuongeza zaidi hatari ya mtu kupata depression
kulingana na shirika la Centre for disease control mtoto aliyepitia viwango vikubwa vya mateso "childhood adversity" kama vile kukua katika familia iliyovunjika,kukua katika familia ambayo mzazi alikuwa mlevi au mtumiaji wa dawa za kulevya ,kukua katika familia ambayo kuna mtu alikuwa na tatizo la akili ,au mtoto kufanyiwa ukatili wa kijinsia au wa kingono yote hayo yanaongeza hatari zaidi ya mtu huyo kupata depression
waligundua hayo katika tafiti za mwanzo kuhusu uhusiano huo utafiti huo uliitwa "Adverse Childhood Experiences (ACE) Study" kulingana na tafiti hiyo mtu mwenye ACE score kubwa zaidi ya 4 anaongeza hatari zaidi hapa chini nimekuwekea kipimo hiko
Angalia ACE score yako ni ngapi?
5.Cause Five: Disconnection from Status and
Respect
mwandishi ameelezea vyema kazi ya Robert Sapolsky na ameelezea namna ambavyo kadri ambavyo matabaka yanavyozidi kuongezeka katika jamii nini kinatokea katika afya za watu kulingana na mwandishi "unapokuwa na jamii yenye matabaka makubwa ya kimapato na hadhi inatengeneza muonekano kwamba watu fulani ni muhimu kuliko wengine na wengine kama hawana umuhimu kabisa "
Jiulize inaleta hisia gani kwa watu wa tabaka la chini? siku hizi tuna mitandao ya kijamii ambayo mtu anaweza kuharibiwa heshima yake ndani ya muda mfupi tu hili nalo japo mara nyingi halitupiwi macho linaweza kuongeza viwango vya depression kwenye jamii
6.Disconnection from the Natural World
kutenganishwa na ulimwengu asilia kwa muda mrefu
Matatizo ya afya ya akili mengi yalionekana zaidi mijini ukilinganisha na vijijini mwandishi anasema athari za kisaikolojia za kutengwa na mazingira asilia zilianza kufanyiwa utafiti miaka michache iliyopita
Kundi la watafiti wa chuo cha Essex huko Uingereza waliangalia afya za akili zaidi ya wakazi 5000 kwa jumla ya miaka 3 waliangalia makundi mwili kundi la kwanza ni lile walilohamia kwenda mijini na kundi la pili ni wale waliohamia vijijini walitaka kujua mabadiliko hayo yanaathirije afya zao za akili
walichokiona ni kwamba kundi la watu waliohamia vijijini walikuwa na viwango vya chini vya depression ukilinganisha na lile kundi la mwanzo ambao walihamia mjini
Shughuli kama vile mazoezi yanaturudisha katika mazingira asilia na kuleta faida zaidi kwa afya ya akili na tafiti zipo wazi pia kwamba upo utofauti mkubwa kati ya mazoezi yanayofanyika ndani (gym kwa mfano) na yale yanayofanyika katika mazingira asilia
ukiachana tu na kwamba binadamu wanapata athari wanapoachana na mzingira asilia wanyama pia huonyesha dalili za depression wanapoondolewa katika mazingira yao asilia
Isabel Behncke ambaye amehojiwa na mwandishi kuhusu wazo hili ni moja kati ya mtafiti aliyefatilia athari hii huyu Isabela alifanikiwa kutembea katika misitu ya kongo alitumia muda wake mwingi akiishi na nyani katika msitu huo akiwasoma Isabel anasema "ni ngumu sana kwa mnyama anayetembea eneo hili kupata depression"
7.Cause Seven: Disconnection from a Hopeful or Secure Future
"Kwa miaka mingi, nilikuwa nimegundua jambo lingine kuhusu huzuni na wasiwasi wangu. Mara nyingi ilinifanya nihisi, kwa namna fulani ya ajabu, kuwa na mtazamo mfupi sana. Ilipokuja, ningeweza tu kufikiria kuhusu saa chache zijazo: jinsi ambavyo zilionekana kuwa ndefu, na jinsi ambavyo zingekuwa na uchungu.Ilikuwa kana kwamba wakati ujao ulitoweka.
mwandishi alisema hayo na aliona hali hiyo hiyo kwa watu wengine waliokuwa na depression
Kukosekana kwa tumaini ni jambo moja ambalo linaongeza zaidi hatari ya kupata depression ni wazi kwamba unapokuwa na tumaini ni ngumu zaidi kuhuzunika sana au kuwa na wasiwasi mkubwa
8.Causes Eight and Nine: The Real Role of Genes and Brain Changes
Mbali na sababu ambazo umeziona mpaka sasa nyingi ulizoziona ni sana kuhusu mazingira na namna ambavyo tunaishi na zipo nyingi zaidi
katika kipengele hiki mwandishi ameelezea kwamba ni kweli yapo baadhi ya mambo katika miili ya watu ambayo inaweza ikaongeza hatari zaidi ya mtu kupata depression kuna baadhi ya watu hurithi gene mbalimbali ambazo zinaongeza hatari hiyo zaidi kwa mfano tafiti zimeonyesha kwamba gene ya 5-HTT imeonekana kuwa na uhusiano na depression kwa watu wenye gene hiyo
Ia ukweli ni kwamba kuwa na gene hiyo haimaanishi kwamba ndio umeandikiwa kwamba utapata depression mara nyingi muunganiko wa gene na mazingira yanayochochea zaidi kuonekana kwa gene hizo husababisha tatizo lenyewe
Hizo ndizo zilikuwa sababu za depression kulingana na Johann Hari
Mpaka sasa umeona sababu sasa una nafasi ya kuimarisha na kurekebisha mambo ambayo unayaona hayapo sawa kulingana na mwandishi ni kwamba tumetenganishwa na vitu ambavyo ni muhimu kwa afya zetu za akili na ni muhimu kuungana navyo tena kuungana tena na kazi yenye maana,kuungana na wenzetu na sio kuwa wapweke ,kuungana na mazingira asilia ambayo tumekuwa tukiyakimbiana .
Mwezi huu ambao ni maalum kwaajili ya afya ya akili lengo letu ni kila mmoja kupata uelewa wa nini cha kufanya mifululizo ya vitabu mablimbali kuhusu mada hii itaendelea kuwekwa hapa na kama kunakitu umejifunza share na mtu wako wa karibu kwa pamoja tuinue kizazi chenye afya njema ya akili


1 comment
Very touching full message you've portrayed.
Congratulations 🎉👏