Toxic culture

 


JAMBO AMBALO LINACHOCHEA MAGONJWA ZAIDI

Jamii ambayo inashindwa kuthamini ujamaa — uhitaji wetu wa kuwa sehemu ya wengine, kutunzana, na kuhisi nguvu ya utunzaji ikituelekea —  Jamii ambayo inageuza uso wake mbali kutoka kwenye kiini cha maana ya kuwa binadamu. Ni lazima magonjwa yatokee.

"Wakati watu wanapoanza kupoteza hisia ya maana na kukosa muunganiko wa kijamii, hapo ndipo magonjwa yanapotoka, hapo ndipo kuharibika kwa afya yetu — akili, mwili, afya ya kijamii — kunapotokea," Bruce Perry mtaalamu wa akili na neva(psychiatrist &neuroscientist)   kama vingepatikana virusi ambavyo vinasababisha athari sawa kwa ustawi wa jamii kama upweke, utengano wa kijamii   habari zake zingejaa  kwenye kurasa za mbele za magazeti. Ila bado tunachukulia athari hizi kikawaida  

Tumezama katika dhana potofu iliyozoeleka kwamba sisi, kila mmoja wetu, ni watu binafsi tu tunaojitahidi kufikia malengo ya kibinafsi. Kadiri tunavyojifafanua kwa njia hiyo, ndivyo tunavyozidi kutengwa na vipengele muhimu vya sisi ni nani na tunahitaji nini ili kuwa na afya. Miongoni mwa wanasaikolojia kuna makubaliano mapana kuhusu mahitaji yetu ya msingi yanajumuisha nini. Haya yameorodheshwa kwa njia mbalimbali kama:

 -Kuwa sehemu ya wengine, uhusiano, au muunganiko wa kijamii;

- Uhuru "autonomy": hisia ya kuwa na udhibiti katika maisha ya mtu;

- Ustadi au uwezo " Mastery 

- kusudi, maana: kujijua kama sehemu ya kitu kikubwa zaidi kuliko  wewe inaweza kuwa ni kiroho..

-"Taarifa kwamba maisha ya kimwili na kiakili ya mwanadamu, na asili , yanategemeana inamaanisha tu kwamba asili inategemeana yenyewe, kwa kuwa mwanadamu ni sehemu ya asili." Hivyo aliandika Karl Marx akiwa na umri wa miaka ishirini na sita mwaka 1844.

Hakuna hata moja ya haya linalokuambia chochote usichokijua au kukihisi tayari. Unaweza kuangalia uzoefu wako mwenyewe: 

Inakuwaje wakati kila moja ya mahitaji hapo juu yanapotimizwa? 

Huwa unajiskiaje ukiona kuna muunganiko mzuri kati yako wewe na wenzako,unapoona una kusudi fulani huwa unajiskiaje? Na mwisho nikuulize 

Nini kinatokea akilini na mwilini mwako yanapokosekana?

Nini kinatokea unapokataliwa? Au kutengwa? Au kuwa mpweke?  

Hakikisha unafanya bidii kutengeneza mazingira yatakayokidhi mahitaji yako ya kisaikolojia  

#Raising healthy generation

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...