Kukabiliana na nyakati ngumu
Inawezekana umefikia hatua ngumu maishani. Mambo hayaendi kama ulivyopanga. Unahisi umekwama
Huenda ni katika kazi yako au kwenye uhusiano. au labda unaona una mwaka mbaya. Au hata siku mbaya
Wakati wowote unapohisi kukata tamaa au kwamba huna bahati au huzuni nyingi, Jaribu hili
Mtafute mtu anayehitaji msaada—labda mtu ambaye pia anahisi maisha yake hayapo vizuri—na mfanyie jambo. Sio lazima iwe jambo kubwa. Ongea naye ,Mpe kinywaji, shada dogo
au mpigie tu simu kumsalimia Mtu huyo hata sio lazima awe mtu unayemjua. Nenda kwenye nyumba ya wazee fanya chochote kitu ambacho kinaweza kuwa na msaada kitu ambacho kitawafanya wahisi kwamba kuna watu wanawaona na kuwajali ,hali zao zikiimarika hali yako inaimarika pia
Mara tu umefanya tendo fulani la fadhili au ukarimu,angalia jinsi unavyohisi baada ya hapo
Je kuna unafuu kidogo? kama sivyo jaribu tena
Utagundua kwamba kadri unavyowapa wengine, ndivyo unavyozidi kujiskia vizuri zaidi
Ulichokisoma hapo juu kinaitwa "helper's high" ni ile hali ya kujiskia vizuri baada ya kuwasaidia wengine unaweza kuitumia vizuri mbinu hiyo kukabiliana na nyakati ngumu
Join the conversation