Labda unapaswa kuongea na mtu
NANI ANAWEZA KUJIKUTA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI?
Afya ya akili ni sehemu muhimu sana katika ustawi wetu wa kila siku sawa kabisa na afya ya mwili. ila sasa, mara nyingi huzungumzwa kwa siri au hata kupuuzwa kabisa. na ukweli ni kwamba, mtu yeyote anaweza kujikuta na changamoto ya afya ya akili, bila kujali umri, jinsia, kabila, au hali ya kiuchumi. Hakuna kinga dhidi ya matatizo ya afya ya akili, na yanaweza kumpata yeyote, wakati wowote maishani. Kuanzia stress za kimaisha, matukio mabaya, magonjwa, hadi mabadiliko ya kibaolojia, zipo sababu nyingi zinazoweza kuchangia kudhoofika kwa afya ya akili.
Hata ambao ni wataalamu waliosomea maswala ya afya ya akili nao kuna wakati hujikuta katika changamoto za afya ya akili
Kwenye kitabu chake cha Maybe You Should Talk to Someone" Lori Gottlieb ambaye ni mwandishi na mtaalamu wa afya ya akili "Psychotherapist" mbali na kuwa anawasaidia watu wenye changamoto za afya ya akili yeye mwenyewe anajikuta akihitaji msaada "therapy"
Kwenye kitabu hiki, tunamwona Gottlieb akifanya kazi kama mtaalamu anayewasaidia wagonjwa wake lakini pia tunaiona safari yake mwenyewe kama mgonjwa anayetafuta msaada. Kuanzie mhitimu wa chuo kikuu anayetafuta maana ya maisha hadi habari ya mzee anayetaka kujiua na yeye mwenyewe Lori anatuonyesha kuwa japo hali zetu za kimaisha hutofautiana Changamoto za msingi tunazokutana nazo zinafanana kwa wote
Mambo Makuu Tunayopambana Nayo kila siku :
Kulingana na Lori Gottlieb, masuala haya muhimu yanatugusa sisi sote:
- Kifo na maana ya maisha: Kukubaliana na ukweli kwamba kuna mwisho wa maisha ,na jambo la muhimu kwa kila mmoja ni kupata maana ya maisha kwani kukosa maana kunakuweka kwenye hatari zaidi ya changamoto kama vile depression
- Huzuni kupoteza: Kupambana na hasara mbalimbali iwe ni mahusiano, kushindwa kutimiza ndoto au kutofikia matarajio yako ,yote hayo huamua pia uimara wetu wa kiakili
- Jinsi ya kupenda na kupendwa: Hasa kwenye kutafuta uhusiano wa kweli na kukabiliana na upweke yote haya ni muhimu mambo haya yanapovurugika utulivu wa akili hupotea
- Mabadiliko ya kila siku na ugumu katika kuyapokea mabadiliko: Kwamba mara nyingi kuna mifumo na utaratibu ambao tumeshauzoea na ikitokea mambo yamebadilika kuna ugumu kwa wengi kuyakubali mabadiliko hayo mfano kupoteza kazi ama vifo vya ndugu
- Hofu ya kuumizwa: Uhalisia kwamba hakuna anayependa kuumizwa na Ugumu n hata wakati mwingine tabia tunazozijenga ili kujikinga na maumivu huishia kutuumiza sisi wenyewe
- Aina ya mawazo na mambo tunayoyaamini kuhusu sisi wenyewe: Mra nyingi kinacholeta maumivu zaidi ni aina ya mawazo ambayo tunayaruhusu katika akili zetu hivyo ni muhimu kuwa na ujasiri wa kuhakikisha ukweli wa mawazo hayo
- Madoa yasiyoonekana : Mara nyingi pia zipo tabia za kila siku ambazo umeshazizoea na kutusababishia maumivu mara nyingi hata bila kujua.
Msisitizo mkubwa katika kitabu hiki ni kwamba japo matatizo yetu yanatofautiana mchakato wa kupambana na matatizo hayo na hasa hisia zinazoambatana na matatizo hayo mara nyingi huwa inafanana
Nini ukifanye sasa?
Safari ya uponyaji ama ili kuweka mambo sawa inaanza kwa kujua ni tatizo gani unakumbana nalo na haihitaji upambane nalo peke yako unaweza ukapata msaada toka kwa watu wako wa karibu na mambo yakakaa sawa
#Pamoja kuimarisha afya #Afya ya akili ni muhimu

Join the conversation