Situational modification

Simu ni muhimu lakini mahusiano yetu na simu yanaamua madhara ya simu na mitandao ya kijamii katika afya zetu na mahusiano yetu ya kijamii

Moja ya mbinu unayoweza kuitumia hasa na matumizi yako ya simu ni situational modification, inaongelea zaidi namna ambavyo kubadili mazingira inaweza kubadili namna ambavyo unaitumia simu yako

  1. Unapohitaji kuzingatia kwa umakini na kazi fulani unaweza ukaweka simu yako sehemu nyingine na sio karibu yako.

    Mbali na muingiliano "distractions" zitakazosababishwa na simu kuwa karibu na wewe, uwezo pia wa ubongo wako kufanya kazi hiyo vizuri unapungua.

    Katika moja ya tafiti ambapo wanafunzi walikuwa wakipimwa vipimo vya IQ, ilionekana kwamba wanafunzi walioweka simu zao karibu wakati wanachukua kipimo cha IQ, matokeo yao yalikuwa chini ukilinganisha na wale ambao hawakuweka simu zao karibu nao.

    Jaribu uone namna ambavyo utaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ukiiweka mbali na wewe kwa muda mchache tu.

    "It's amazing how much you can get done if you work for 12 hours without your phone" Alex Hormozi

  2. Siku nyingine ukiboeka ama ukihisi upo mpweke badala ya kufikia simu yako fanya hivi:

    Toka nje tembea.

    Mnamo Agosti 22, 1853, Henry David Thoreau alitafakari kwa kina juu ya jaribio lake la miaka miwili la kuishi Walden Pond. Aliamua kuishi Walden Pond kwa miaka miwili kama jaribio. Aliamini watu wengi huishi maisha yenye haraka na yasiyo na maana, na alitaka kutafuta maana halisi ya maisha bila kuathiriwa na shinikizo za jamii na mali. Pia alitaka kupata muda wa utulivu peke yake bila usumbufu mwingi.

    Siku hiyo aliandika jambo ambalo lina ukweli zaidi leo: "All nature is doing her best each moment to make us well. She exists for no other end, do not resist her. With the least inclination to be well, we should not be sick."

    Alimaanisha kwamba "Asili yote inafanya jitihada zake zote kila wakati kutufanya tuwe wazima. Haipo kwa lengo lingine, usiikaidi. Kwa mwelekeo mdogo tu wa kutaka kuwa wazima, tusingeugua."

    Kwa bahati mbaya, wachache sana kati yetu wanazingatia ushauri wa Thoreau.

    Siku hizi, kadri siku zinavyokwenda, muda unaotumiwa katika mazingira asilia ama nje unazidi kupungua na haitufaidishi chochote.

    Ni wewe tu ndio unayejua muda unaoutumia nje, na ni wewe tu unaweza kuubadilisha.

  3. Unapokuwa katika mazungumzo na wenzako ama ukiwa unakula na wenzako fanya hivi:

    Weka simu mbali ama ifiche. Ni mara ngapi umekuwa katika mazungumzo na mwenzako ila hukuwa unamsikiliza kwa umakini ulikuwa bize kujibu meseji fulani?

    Ndio, simu zinaweza kutuweka pamoja na kutuunganisha na tuwapendao lakini simu hizo hizo zinaweza kutuiba na kutuenga mbali na watu wetu wa karibu.

  4. Jaribu kutokuweka simu yako kitandani unapokwenda kulala.

    Ukiachilia mbali kwamba muda ambao tunalala umezidi kupungua, ubora wa usingizi pia unazidi kuharibika kwani tumebeba mikononi mwetu kifaa ambacho kinachochea hilo kwani huharibu ubora wa usingizi tunaoupata.

    Ili uhakikishe unapata usingizi bora, usiende na simu kitandani. Jaribu kuiacha katika chumba kingine au ifiche hadi asubuhi badala ya kupanda nayo kitandani.

Mbinu hizi zinaweza kukusaidia kwa kuanzia. Mbinu zingine zitaendelea kutumwa zaidi, hivyo endelea kutufuatilia na utakapohitaji msaada usisite kuripoti.

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...