Anxiety inaonekanaje? Ama Ipoje?

 Anxiety (wasiwasi) 

Kikawaida ni hali inayokupata hasa huja kama uoga kutokana na tukio ama jambo lililopo mbele yetu au wakati mwingine jambo ambalo tunahisi linakuja kutukabili 

Hali hii inatusaidia nini hasa maisha yangeeda vizuri usingekuwa unaogopa sio?

wasiwasi unatusaidia nini hasa ,Fikiria hii wakati mwingine wasiwasi juu ya jambo fulani inatufanya tulizingatie zaidi ili mambo yaende vizuri mfano kwa upande mmoja wasiwasi juu ya mtihani unaweza kukusukuma kusoma kwa bidii ili ufanye vizuri 

Lakini mara nyingine wasiwasi huwa tatizo kisaikolojia na linaweza kuleta madhara inakuwa ugonjwa wa akili ,mtu anakuwa na uoga usio wa kawaida na unaathiri ubora wa maisha yake na hali yake ya kiakili ikifikia hatua hiyo utaskia mtu ana "anxiety disorders"

Hali hii inaweza kuonekana kwa namna tofauti kwa watu wawili kwani zipo aina nyingi ,aina zake hizi hapa,

 1.Generalized anxiety disorder :hofu inapovuka mipaka

Hapa mtu anakuwa na uoga usio halisi mfano paka akilia usiku mtu anaona kama kuna tatizo,kuogopa kama kuna watu wanakufuatilia na wanataka kufanya kitu kibaya  wakati mwingine anashindwa hadi kulala. Kukasirika haraka hata kwa mambo madogo, kuwa na tahadhari kupita kiasi ni kama anajiandaa mda wote maana kuna kitu kibaya kinaweza kutokea 

2.Panic disorder 

Hapa ni utaona hofu za ghafla na za kujirudia-rudia ,utashangaa tu mtu anashtuka usiku na kupiga makelele ,mapigo ya moyo kwenda kasi ,hofu kali kwamba unataka kufa,hudumu kwa muda hadi dakika 10 

 3.Phobia

Hapa ni hofu juu ya kitu fulani ,inaweza kuwa ni hofu ya watu(social phobia) utaona mtu anaepuka mazingira yenye watu au Moyo kwenda mbio, kutetemeka, kutokwa jasho, au kuhisi kichefuchefu unapokuwa katika hali za kijamii ,wakati mwingine phobia inaweza kuwa ni juu ya vitu husika labda wanyama fulani au damu ,moja ya mbinu inayotumika kuwasaidia watu hapa ni exposure therapy ambapo mtu anaongozwa kuelekea kile kitu anachokiogopa sana labda anaogopa mdudu fulani ,ataanza kuonyeshwa mdudu huyo kwenye TV , kadri muda unavyokwenda ataonyeshwa mdudu huyo kwa ukaribu zaidi hadi hofu itakapoisha mbinu hii hutumika pia kwa PTSD ambayo utaiona hapo mbele

4.Obsessive—compulsive disorder (OCD)

Hili hasa ni tatizo la kulazimishwa kufanya kitu mara kwa mara utaona mtu ,mtu anatawaliwa na mawazo yanayompa wasiwasi juu ya mambo fulani mfano kukagua kila mara kama mlango umefungwa (inaweza kujirudia zaidi ya mara 10) au kunawa mikono mara kwa mara isivyo kawaida 

5.Posttraumatic stress disorder 

Hii hasa hutokea baada ya wewe kukutana na tukio la kutisha labda ilitokea ajali ,akilini tukio linajirudia kila mara , kuepuka maeneo yanayohusika na tukio lenyewe ,kupoteza hamu ya kufanya mambo uliyofurahia hapo mwanzo ,kuchukia kundi fulani la watu utakuta mdada anachukia au kwuaogopa wanaume sababu labda hapo nyuma alifanyiwa jambo baya na mwanaume 

Mwaka 2019 shirika la afya duniani (WHO) walikadiria kwamba watu takriban milioni 301wanakutana na tatizo hili, Kwanini baadhi ya watu wanakumbana na tatizo hili ? tutaangazia zaidi katika toleo lijalo

Ikiwa mtu ana tatizo moja wapo hapo juu zipo njia mbalimbali za kimatibabu ambazo zinaweza kutumika ikiwemo dawa,na therapy usisite kutafuta msaada 



  

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...