Bipolar disorder :Ukiona ishara hizi


Dalili za Bipolar disorder

Ugonjwa huonekana kuwa na nyakati mbili ,nyakati za hisia za juu unakuta mtu ni mchangamfu kupitiliza na nyakati zingine uchakamfu unaisha 

Mfano utaona nguvu ziliongezeka isivyo kawaida ,wakati mwingine ongezeko la hisia kali kama vile hasira, hudumu kwa angalau wiki 1 zifuatazo ni baadhi ya dalili zake 

  1. Kujithamini kila mara kupita kiasi na kujiamini kupita kiasi  (yaani hapa utaona mtu ana imani kubwa kupitiliza ,anaamini"naweza kufanya chochote" ,kujiongezea umuhimu kupitiliza utakuta anaamini kwamba kakutana na watu wakubwa)

  2. Kupata changamoto ya usingizi (mfano anahisi kwamba baada ya kulala tu masaa 3 anaona ameshapumzika).

  3. Kuongea sana kuliko kawaida au shinikizo kutaka la kuendelea kuongea zaidi.

  4. Mawazo yanayoruka-ruka au kuhisi kwamba mawazo yako yanakimbia kila wakati.

  5. Kupoteza umakini kwa urahisi (yaani umakini kupotea na kupotelea kirahisi kwenye mambo mengine yasiyo  muhimu au yasiyohusika kwa wakati huo).

  6. Kuongezeka kwa harakati zinazoelekezwa kwenye lengo fulani (inaweza kuwa  kijamii, kazini au shuleni, unakuta mtu ghafla ana lengo fulani analifukuzia sana wka muda huo kupita kiasi,ghafla tu mtu anajihusisha na mambo mengi kwa wakati mmoja kwa nguvu sana) 

  7. Kushiriki sana kwenye mambo ya burudani au  kufurahisha ambayo yana uwezekano mkubwa wa kuleta matatizo zaidi  (Inaweza kuwa ni  matumizi makubwa ya ya pesa ,ngono,uzinzi, au uwekezaji fulani )

 Kwa kuzijua dalili hizi unaweza kutambua mapema na kutafuta msaada kwako au kwa watu wako wa karibu 

Tupe maoni yako ya kile unachotaka kukijua zaidi 

 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...