Njia 4 za Kuboresha Usawa wa Homoni na Afya ya Akili

Homoni zikikosa usawa, nawe pia utajisikia vibaya. Dalili nyingi za matatizo ya homoni hufanana na zile za matatizo ya afya ya akili. Ndiyo maana wakati mwingine changamoto kama sonona au wasiwasi (anxiety) zinaweza kusababishwa na mvurugiko wa homoni. Hali hizi za homoni zinaweza kukosewa na kuonekana kama magonjwa ya akili kwa sababu mara nyingi dalili zake hufanana.

Mwilini mwako zinazalishwa homoni nyingi na zina mchango kwenye utendaji kazi wa ubongo kwa kiasi kikubwa ni kama vile homoni ya thyroid, cortisol (homoni ya stress),homoni ya insulin,homoni ya estrogen ,progesterone zote hizi kwa namna moja ama nyingine huathiri mood,uchangamfu,stress na hivyo basi inapotokea hakuna usawa mambo hayatakwenda vizuri kama katika hali hizi hapa

  • Viwango vya chini vya homoni ya thyroid huwa na dalili kama vile uchovu,kusahau,huzuni,kushindwa kuzingatia pia watu hawa wapo katika hatari zaidi ya kupata sonona "depression"
  • Kinyume chake homoni ya thyroid inapozalishwa kwa wingi zaidi mtu anakuwa na wasiwasi kupita kiasi, mwenye hasira, asiye na utulivu, na mwenye mawazo yanayokimbia yanayomzuia kulala. Anaweza kuhisi yuko hatarini kila wakati, akipata hofu (panic attacks), au hata kuwa na dalili zinazofanana na mania au ugonjwa wa wasiwasi wa jumla (generalized anxiety disorder)
  •  Mabadiliko ya Ghafla ya Estrogen (Wanawake):Wanawake wengi hupata mabadiliko ya hisia kabla ya hedhi, kuwashwa, na huzuni.Mabadiliko haya makubwa yanatokana na kushuka ghafla na kubadilika-badilika kwa viwango vya estrogen na progesterone, huku yakiathiri moja kwa moja ubongo pia kipindi cha  Menopause wanawake hupitia vipindi vya wasiwasi mkali na huzuni kali pia 
  •   Kushuka kwa Testosterone (Wanaume): Kama vile wanawake wanavyopata mabadiliko ya homoni, wanaume pia hupata na kadiri viwango vya testosterone vinavyopungua polepole kadri umri unavyoongezeka  wanaume kama wanaweza kujikuta wakipata uchovu usioelezeka, kupungua kwa kiasi kikubwa kwa hamu ya tendo la ndoa, kuongezeka kwa kuwashwa, na hisia za kudumu za huzuni zinazofanana na mfadhaiko.  
  •  Viwango vikubwa vya homoni ya stress 'cortisol" vimeonekana pia kuwa na uhusiano mkubwa na sonona 

 Mambo gani yanaweza kusababisha mvurugiko wa homoni?  

Usawa wa homoni ni muhimu kwa afya yetu kwa ujumla, lakini mambo mbalimbali yanaweza kusababisha usumbufu huu. Hali kama vile msongo wa mawazo sugu na viwango vya juu vya homoni ya cortisol (homoni inayohusika na stress) Lishe duni pia ina jukumu kubwa; ulaji mwingi wa sukari na wanga pamoja na upungufu wa virutubisho muhimu kama vile vitamini B12, B9, A, B6, C, chuma, iodini, zinki .Uzito kupita kiasi (obesity) na matatizo ya kiafya yanayoendelea kama vile magonjwa sugu mfano kisukari au utendaji mbaya wa ini na figo, zote zinaweza kuathiri uzalishaji na usawa wa homoni mwilini.


Njia 4 za Kuboresha Usawa wa Homoni na Afya ya Akili

Usawa wa homoni una athari kubwa kwa afya ya ubongo na akili ni muhimu kuelewa jinsi homoni zinavyofanya kazi na nini cha kufanya kuziboresha.hapa zipo hatua nne muhimu unazoweza kuchukua ili kuboresha usawa wa homoni zako na  afya yako ya akili

1. Dhibiti Msongo wa Mawazo (Stress)

Msongo wa mawazo sugu huongeza homoni ya cortisol, ambayo inaweza kuvuruga homoni zingine nyingi mwilini mambo haya yanaweza kukusaidia 

  • Fanya mazoezi ya kupumua kwa kina(Deep breathing): Hii husaidia kukutuliza na kuthibiti msongo wa mawazo

  • Tafakari (Meditation): Dakika chache kwa siku za kutafakari zinaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha hisia.

  • Lala vya kutosha: Ukosefu wa usingizi huongeza msongo wa mawazo na kuvuruga homoni. Pata usingizi bora kila usiku.

  • Jihusishe na shughuli unazopenda(Hobbies): Mamabo ambayo unaya enjoy soma kitabu, sikiliza muziki, au fanya chochote kinachokuletea furaha na kukupumzisha.

2. Zingatia Lishe Bora na Kamili

Chakula unachokula huathiri moja kwa moja uzalishaji na usawa wa homoni.

  • Punguza sukari na wanga : Hivi vinaweza kukuongezea hatari ya kupata magonjwa sugu kama viel kisukari ambayo yanaathiri usawa wa homoni  

  • Kula protini za kutosha: Protini ni muhimu kwa ajili ya kujenga homoni. Jumuisha vyanzo vya protini kama nyama ,samaki, mayai, maharage, na karanga katika milo yako.

  • Ongeza mafuta yenye afya kama vile omega 3: Mafuta kama yale yanayopatikana kwenye parachichi, samaki wenye mafuta (salmoni), karanga, na mbegu husaidia katika uzalishaji wa homoni.

  • Hakikisha unapata virutubisho muhimu: Zingatia kupata kiasi cha kutosha cha vitamini B12, B9, A, B6, C, chuma, iodini, na zinki kupitia chakula au virutubisho kama ikihitajika

3. Fanya Mazoezi Mara kwa Mara

Mazoezi ya wastani na endelevu yana faida nyingi kwa usawa wa homoni ikiwemo ..

  • Inasaidia kudhibiti uzito: Uzito kupita kiasi (hasa mafuta tumboni) unaweza kuvuruga homoni kama vile estrogen na testosterone.

  • Inapunguza msongo wa mawazo: Mazoezi husaidia kupunguza viwango vya cortisol.

  • Inaboresha ufanyaji kazi wa insulin: Hivyo huimarisha udhibiti wa viwango vya sukari ya damu

  • Inaboresha mzunguko wa damu: Hii husaidia homoni kusafirishwa vizuri mwilini.

4. Fanya Uchunguzi wa Afya Mara kwa Mara na Ongea na Mtaalamu

Kumbuka huwezi kujua kama una matatizo ya homoni bila kupimwa.

  • Pima viwango vya homoni zako: Ongea na daktari wako kuhusu kupima viwango vya homoni ya thyroid , homoni zingine (estrogen, progesterone, testosterone), na cortisol, hasa kama unapata dalili za mfadhaiko, wasiwasi, au matatizo mengine ya akili 

  • Tafuta ushauri wa kitaalamu: Daktari au mtaalamu wa lishe anaweza kukusaidia kubaini chanzo cha matatizo ya homoni na kukupatia mpango wa matibabu au ushauri wa binafsi 


Swali kwako : Njia 4 zote hapo juu huenda umeshawahi kuzisikia au tayari unazifahamu  kama ambavyo wengine wengi wanafahamu, kitakachokutofautisha ni uwezo wako wa kuchukua hatua chagua jambo moja kisha jiulize ni hatua gani ndogo naweza kuchukua leo?
Hongera kwa kuijali afya yako 

Je una maswali kuhusu afya ya akili? au kuna jambo ungependa kulijua vizuri zaidi kuhusu afya yako? endelea kuwasiliana nasi 

 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...