Fanya hivi kupunguza shinikizo la juu la damu




Kama ilivyo michakato mingine mwilini presha ya damu haipaswi kuwa kubwa sana au ndogo sana inapokuwa ndogo sana kwa mfano seli mwilini kwako zitakosa oxygen na ikiwa kubwa sana inaleta uharibifu wa mishipa 

Kwanini ni muhimu kujua kuhusu shinikizo la juu la damu? 

Shinikizo la juu la damu kwa jina lingine "hypertension" mara nyingine huitwa "silent killer" sababu kikawaida hauna dalili na watu wengi wanaweza kuwa na tatizo hili kwa miaka mingi bila kujua huku ukiendelea kusababisha madhara mengi mwilini ukiacha bila kutibiwa utasababisha madhara kama vile kiharusi "stroke" magonjwa ya figo ,magonjwa ya moyo na mengine mengi  

Namna ya kupunguza shinikizo la juu la damu 

Kwa watu wengi wanaweza kupambana na shinikizo la juu la damu kwa kuzingatia mbinu mbalimbali zinazolenga mitindo ya kimaisha na tabia za kila siku hasa kujikinga na pia utumiaji wa dawa   haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukusaidia kukabiliana na tatizo hili

 1. Zingatia kuwa katika uzito wa wastani  

  • Uzito mkubwa inaongeza hatari zaidi ya kupata shinikizo lajuu la damu na imeonekana katika tafiti nyingi kwamba kupunguza uzito huleta mabadiliko katika shinikizo la damu

  • Mbali na kuongeza hatari ya shinikizo la juu la damu uzito mkubwa huongeza hatari ya magonjwa sugu mengine

2. Zingatia kufanya mazoezi mara kwa mara 

  • Chochote kile ambacho unakifanya kama mazoezi yako ikiwa ni kuruka kamba ,kukimbia,vyuma (weights) ,kutembea vyoye hivyo vinaweza kusaidia kuimarisha mishipa yako ya damu na kuimarisha afya ya moyo  

3. Zingatia milo yenye afya Eat a Healthy Diet:

  • Kipengele cha chakula ni muhimu sana zingatia milo yenye matunda mbogamboga za kutosha 

  • Aina ya diet kwa jina la DASH diet (Dietary Approaches to Stop Hypertension) imeonekana kusaidia sana kupunguza presha ya damu unaweza ukaelekezwa na daktari wako 

  • Punguza ulaji wa chumvi nyingi zaidi 

4. Punguza unywaji wa pombe  na epuka uvutaji wa sigara 

  • Matumizi ya pombe kwa wingi yanachangia ongezeko la shinikizo la juu la damu


7. Thibiti msongo wa mawazo:

  • Msongo mkali wa mawazo unachangia sana shinikizo la damu  

  • Hivyo angalia njia mbalimbali za kuthibiti stress kama vile mazoezi,kupata muda na marafiki,au kufanya mambo unayoyapenda 

8. Pata usingizi wa kutosha.

9.Kupima mara kwa mara presha ya damu na pia kupambana na tatizo linapoonekana mapema

 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...