Protein powder: Je ni lazima kutumia?

Huenda umewahi kupata changamoto kujua aina zake au labda huzijui hujui kabisa ,ni kwaajili gani ? kazi yake ni nini? haupo peke yako kwanza tujue zina kazi gani

Tupate historia yake kidogo :Zilianzia wapi?

Protein powder ya kwanza ilitumika na madaktari kuwasaidia wagonjwa ambao walikuwa na changamoto za tumbo na wale ambao walikuwa na matatizo ya kupoteza misuli  

ila miaka ya 1900 ilianza kutumiwa na wanariadha ,wasanii hasa wa "Hollywood" kama njia ya kuongeza misuli protein powder ya kwanza kutumika ilikuwa ni ya mayai (yaani egg based protein) baada ya apo aina zingine nyingi ziliendelea kuzalishwa 

Protein powder ni virutubisho maarufu vya lishe vinavyotumika kwa malengo mbalimbali kama vile kujenga misuli, kudhibiti uzito, au tu kuongeza kiwango cha protini mwilini hasa kwa watu ambao hawapati kiwango cha kutosha kwenye mlo wa kila siku 

Protini ni kirutubisho kikuu cha muhimu kwa kila mtu, bila kujali jinsia (wanawake ,wanaume wote wanatumia)

Tofauti kuu kati ya protein powder hutokana na chanzo chao na jinsi zinavyosindikwa.

 Protini Zinazotokana na Wanyama

Poda hizi hutoka kwa wanyama mfano maziwa, mayai, au nyama na mara nyingi kundi hili ni protini kamili 

Protini ya Whey (Whey pritein)

Whey ni protini bora na kamili inayotokana na maziwa  zipo aina mbalimbali pia

  • Whey Protein Concentrate (Whey Concentrate): Aina hii ni ile isiyosindikwa sana. Ina 70-80% ya protini, pamoja na mafuta, wanga, na lactose. Ni nzuri kwa ujumla wa kujenga misuli na kutumika kama chanzo cha protini

  • Whey Protein Isolate (Whey Isolate): Hii husindikwa zaidi ili kuondoa mafuta na wanga, na hivyo protini huwa kwa wingi 90%. Ni chaguo zuri  kwa kujenga misuli,kupunguza uzito,na pia kukupa kiwango sahihi cha protini kulingana na mahitaji ya mwili wako  

Zingine Zinazotokana na Wanyama ni

  • Protini ya Casein: Pia inatokana na maziwa Wanariadha wengi hutumia kabla ya kulala ili kuzuia misuli kudhoofika.

  • Protini ya Yai: Chanzo bora cha protini kamili ambacho humeng'enywa polepole zaidi kuliko whey. Ni chaguo bora kwa watu wenye allergy ya maziwa  

Protini za Mimea 🌱

Kwa wale wanaotaka kuepuka bidhaa za wanyama(Vegans) au wanapendelea tu lishe ya mimea, kuna chaguzi nyingi nzuri pia.

  • Protini ya Pea(Pea protein): Hii ni chaguo ambalo humeng'enywa kirahisi na haisababishi allergy ila aina hii sio protein kamili kwa hivyo mara nyingi huchanganywa na protini zingine za mimea ili kuikamilisha

  • Protini ya Mchele wa Kahawia(Brown rice protein): Hii ni protini ya 100% ya mimea,  nayo pia inameng'enywa kirahisi. Ni nzuri kwa mtu yeyote mwenye allergy ya maziwa

  • Aina zingine huwa ni mchanganyiko wa aina mbili za hapo juu

Usichohitaji
Ingawa bidhaa zingine zimejaa vitamini za ziada, madini, na vitu vingine ni muhimu kuzingatia mambo ya msingi zaidi na  jambo la muhimu zaidi ni protini yenyewe. Viungo vingi vya ziada vinaweza kupatikana kwenye vyakula vya kila siku na kumbuka kwamba protini powder inayokufaa inategemea mahitaji yako ya lishe, malengo, na mapendeleo yako binafsi

Je ungependa post zijazo zihusu nini ? tuambie 

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...