Unayopaswa kujua kuhusu allegy ya maziwa
Wapo baadhi ya watu ni kama wana mzio "allergy" na maziwa hali hii inatokana na nini hasa? je umewahi kuona kwamba ukishakunywa maziwa unapata matatizo kama kutapika na kuharisha?basi huenda unakutana na kile kinachofahamika kama "lactose intolerance"
Hali hiyo inaitwa "lactose intolerance" Ni pale ambapo mtu hawezi kumeng'enya lactose(ambayo ipo katika maziwa na bidhaa zake) kushidikana kwa mmeng'enyo wa lactose unaweza kuonekana kwa baadhi ya dalili kama vile
👉Kuharisha,
👉tumbo kujaa gesi
👉Kutapika
👉Maumivu ya tumbo
Kwa Nini Hii Hutokea? Sababu sababu za lactose intolerance
Hapo juu ni baadhi tu ya dalili ambazo zinaonekana kinachotokea ni kwamba "enzymes" Ambazo zinatakiwa kufanya kumeng'enya lactose hazizalishwi vya kutosha na mara nying inaweza kuwa ni hali ya kurithi ama umri pia unachagia kwani kwa wengi enzymes hizo huwa zinafanya kazi vizuri tukiwa wadogo tunapokua ufanisi wake unapungua kwa watu wengi ndio maana wanakuwa katika hiyo hali na baadhi ya watoto huzaliwa wakiwa hawana uwezo wa kumeng'enya lactose hivyo huweza kuonyesha mzio wa maziwa pia na bidhaa zingine za maziwa
Ufanye nini sasa?
Jambo la muhimu ni kufanya vipimo kama kweli unakutana na hali hii na baada ya hapo jitahidi kuangalia mbadala wa maziwa na bidhaa nyingine za maziwa ili kujiepusha na shida zinazoambatana na tatizo hili
kumbuka pia kufuata ushauri wa daktari/mtaalamu wa tiba
https://heallthtipstalks.blogspot.com/2025/02/fanya-haya-kuimarisha-afya-ya-tumbo-gut.html
.png)
Join the conversation