Mentally strong people
Amy Morin ana mengi ya kutueleza kuhusu "mentally strong people" alipokuwa na miaka 23 Mama yake mzazi alifariki siku zote Mama yake alikuwa mkakamavu,mchangamfu na mwenye furaha ya maisha Ilimuweka Amy katika wakati mgumu sio kwamba tu ata mmisi mama yake ila ni kwamba hatomuona tena kilikuwa ni kipindi kigumu kwake na kwa kuwa alikuwa mtaalamu wa maswala ya afya ya akili (mental health practitioner) Amy alielewa kwamba hatoweza kuwasaidia wengine kama hajaweza kutatua hali anayopitia yeye
Kutokana na mafunzo aliyopitia hapo nyuma alielewa kwamba Muda peke yake hautoleta uponyaji kinyume na kile ambacho wengi husema kwamba "time heals" kwake ilikuwa wazi kwamba ni kile anachokifanya na muda ndicho kitakacholeta uponyaji "healing"
Tofauti kabisa na trends tunazotupiwa mitandaoni kila mara za "be positive" ambazo kwa mtazamo mkubwa ni kama zinafanya watu kuepuka nyakati za maumivu na kuwa kama vile hakuna hisia nyakati hizi Amy alielewa kwamba lazima apitie nyakati za uchungu alijiruhusu kujiskia vibaya,kuhisi huzuni,kupata hasira,na kukabiliana na ukweli kwamba amempoteza mama yake yaliyobaki ni historia
yafuatayo ni mambo ambayo mentally strong people hawayafanyi
1.THEY DON’T EXPECT IMMEDIATE RESULTS
Tafsiri: Hawategemei matokeo ya haraka haraka
Patience, persistence and perspiration make an unbeatable combination for success. —NAPOLEON HILL
tupo katika kipindi ambacho mambo mengi ni ya haraka fast foods fast internet na kibaya zaidi kwa kuwa mambo yapo kasi tunakwenda na mtazamo huo huo katika mambo yanayohitaji uvumilivu wa hali ya juu napo tunategemea matokeo yawe delivered haraka haraka
Amy anatukumbusha kwamba japo tunaishi katika ulimwengu wa haraka hatuwezi kupata kila kitu haraka
siku zote kuna habari za mtu ambaye amekuwa maarufu haraka sana na tunataka kuwa kama yeye au habari za mtu aliyeanzisha biashara fulani mwezi uliopita saivi ana matawi saba na tunataka matokeo ya haraka kama hayo tunakurupuka na kuishia njiani
elewa kwamba tunaishi katika ulimwengu wa haraka hatuwezi kupata kila kitu haraka
2.THEY DON’T WASTE TIME FEELING SORRY FOR THEMSELVES
Tafsiri: Hawapotezi wakati kujihurumia
mwandishi amemnukuu JOHN GARDNER akisema kwamba "Self-pity is easily the most destructive of the non-pharmaceutical narcotics; it is addictive, gives momentary pleasure and separates the victim from reality"
mwandishi anauliza kwamba kama kujionea huruma ni vibaya kwanini kila mara tunajikuta katika hali hiyo? anasema tatizo hilo litakufanya kuchelewa kukabiliana na kupambana na matatizo yaliyopo mbele yako kila mara na anasema kwamba wengi huitumia mbinu hii ili kutafuta "attention" nukuu " People often use self-pity as a way to gain attention. Playing the “poor me” card may result in some kind and gentle words from others—at least initially"
na anasema kwamba wakati mwingine "self pity" hutumika kama kifaa cha kujilinda nacho na kufanya tuonekane watu wa tofauti na kuhitaji jamii ituchukulie kwa utofauti lakini mbinu hiyo haisaidii kwani kuna majukumu tutakuwa tunayakimbia kwa kisingizio cha kutaka kuonewa huruma
Mwandishi anasema tuache kujionea huruma :madhara yake ni makubwa kwani inatuzuia kukabiliana na matatizo anakwenda mbali zaidi na kusema kujionea huruma ni upotezaji wa muda.
baadhi ya mawazo yanayochangia self pity kulingana na mwandishi ni kama haya kuwaza kwamba Mambo mazuri yanatokea kwa watu fulani peke yake,Maisha yangu yanakuwa mabaya kila,Hakuna anayeweza kukabiliana na jambo hili
Mwandishi anasema ukiacha kujionea huruma na kuchukua hatua utakuwa imara zaidi
3.THEY DON’T WORRY ABOUT PLEASING EVERYONE
Tafsiri:Hawajali kuhusu kumridhisha kila mtu
mwandishi amemnukuu LAO TZU mwandishi wa kitabu cha Art of war kwamba
"Care about what other people think and you will always be their prisoner." —LAO TZU
akimaanisha kwamba Jali kuhusu wengine wanachofikiria na siku zote utakuwa mtumwa wao
People pleasing Je yoyote kati ya sifa hizi inahusiana na wewe? Unahisi kwamba unahusika na namna ambavyo wengine wanajiskia? ni rahisi zaidi kwako kukubaliana na mambo hata kama ndani hukubaliani nayo? unaomba msamaha kila mara hata kama huna kosa? siku zote huwaambii watu kama umeumia/wamekuumiza/hujapenda walichofanya kwa kuogopa watakavyokuona? kila mara unatafuta kusifiwa? tabia hii ni hatarishi 'toxic"
kamaalivyoweka wazi katika kitabu chake cha "The Top Five Regrets of the Dying,Bronnie Ware ambaye alifanya kazi na watu wengi ambao walikuwa karibu kufa wengi wao walijutia tabia ya kutaka kumridhisha kila mtu kwamba waliona ni heri wangeishi uhalisia badala ya kutaka kumridhisha kila mtu
4. THEY DON’T GIVE AWAY THEIR POWER
Tafsiri yake:Hawaruhusu wengine kuwanyang'anya nguvu/mamlaka yao
Mwandishi amemnukuu Dale Carnegie "When we hate our enemies, we are giving them power over us: power over our sleep, our appetites, our blood pressure, our health, and our happiness."
hii ni kama una tabia ya kulalamikia kila jambo linalotokea kwenye maisha yako unayemlalamikia ndiye unayempa mamlaka juu ya tatizo au hali unayoipitia mwandishi anaonyesha kwamba tatizo la mtazamo huu ni kwamba unawapa watu wengine kuamua hisia zako,unajiweka katika nafasi ya muhanga kila mara "victimhood mindset" ,unajiondoa katika jukumu la kutatua kile unachokutana nacho kwani unaona unayemlalamikia ndio alipaswa kufanya jambo hilo unakuwa mhanga mkubwa wa upingamizi toka kwa watu wengine "critism"
Amy anatuambia kwamba tunapaswa kurejesha mamlaka yetu toka kwa watu ambao tumewapa iwe ni kwa kujua au kutokujua
mfano kuna mtu kakukosea na hujataka kumsamehe na kila mara unaumia kwasababu ya huyo mtu kwahiyo hapo ni umempa mtu huyo nguvu juu yako umempa hisia zako umempa maisha yako na unavyoendelea kutokumsamehe na kumuondoa moyoni utaendelea katika hali hiyo hiyo mwandishi anasema kusamehe kunasaidia kukupunguzia msongo wa mawazo
5. THEY DON’T SHY AWAY FROM CHANGE
Tafsiri yake: Hawaoni aibu kubadilika
mwandishi ameweka nukuu hii hapa mwanzoni kwamba It’s not that some people have willpower and some don’t . . . It’s that some people are ready to change and others are not. —JAMES GORDON
kwamba sio kwamba watu fulani wana uwezo wa kubadilika na wengine hawana uwezo huo ni kwamba baadhi ya watu wapo tayari kubadilika na wengine hawapo tayari
kwanini mara nyingi watu hawapo tayari kubadilika? unajua kwamba unapaswa kufanya mazoezi kwanini hujaanza? mwandishi ameweka wazi kwamba ni kwa sababu tunaona mabadiliko ni magumu au yanaweza yasidumu au tumejaribu na hatujaona matokeo ya haraka tukakata tamaa mapema
tatizo la kutokutaka kubadilika ,Utabaki pale pale,Hutaweza kuanza tabia nzuri za kiafya,Kadri unavyosubiri inazidi kuwa ngumu zaidi "healthy habits"
Mwandishi anahimiza kukubaliana na mabadiliko japo wakati mwingine ni magumu kwa mfano wewe kuanza kufanya mazoezi mazoezi yanaonekana ni magumu wakati unayafanya ila kuna hali ngumu zaidi inaweza ikakupata huko mbeleni unapoyakosa mazoezi kwahiyo chagua maumivu gani unayotaka
6. THEY DON’T FOCUS ON THINGS THEY CAN’T CONTROL
Tafsiri yake:Hawaweki nguvu nyingi katika mambo yaliyo nje ya uwezo wao
Mwandishi anahimiza kua moja ya jambo muhimu sana ni kuelewa kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako na kile ambacho kipo nje ya uwezo wako mfano Labda umechelewa kwenda kazini na upo unasubiria gari kwaajili ya usafiri na limechelewa kutokana na mvua hakuna kiwango cha hasira ,na kelele kitakachoweza kutuliza mvua na kukufanya uwahi kazini hilo lipo nje ya uwezo wako
Hakuna kiwango cha matarajio ambacho kinaweza kukufanya wewe kuwa mrefu zaidi /mfupi au kuzaliwa katika nchi nyingine
na haijalishi utafanya nini huwezi ukamfanya mtu akupende na juu ya hayo ni vyema ukaacha kujiumiza kwa mambo ambayo huwezi kuyasogeza badala ya kupoteza muda kwa mambo usiyoweza kubadili ni vizuri ukautumia kwa mambo unayoweza kuyabadili la sivyo tutakuwa tunapigana vita tusiyoweza kushinda "unwinnable battle"
mwandishi anasema kwamba tuna tabia ya kutaka kuwa na mamlaka juu ya kila kitu anasema kujaribu kufanya hivyo kutakuongezea hofu zaidi kutakupotezea muda
Elewa mambo yaliyo ndani ya uwezo wako.
Malizia sehemu ya pili kwa kubonyeza hapa sehemu ya pili

Join the conversation