Ongezeko la changamoto za afya ya uzazi kwa wanaume nini sababu na nini kifanyike?



 
Ongezeko la matatizo ya uzazi kwa wanaume
Afya ya uzazi kwa mwanaume labda kwako ni sentensi ambayo inakushangaza sababu kama wengi umekuwa ukidhani kwamba swala la afya ya uzazi sana linahusu wanawake na hata ukijaribu kutafuta vikundi ambavyo vinahusiana na swala la afya ya uzazi kwa wanaume 


Ongezeko la matatizo ya uzazi kwa wanaume

"Afya ya uzazi kwa mwanaume" ni sentensi ambayo hata wewe inakupa changamoto kuielewa kwani kwa miaka mingi umekuwa ukiamini swala la uzazi sana linahusu wanawake pekee ,nayo haishangazi uliwahi kusikia "Men's fertility support group"? ni ngumu kuyapata makundi hayo sababu ya mtazamo ambao tayari upo katika jamii inayohusisha kuwa mwanaume na ile kuwa na nguvu nyingi na uwezo mkubwa mtazamo huu ukiwaacha wanaume wengi na ugumu wa kukiri kwamba wanapitia matatizo haya wengi huona aibu kukiri au kutafuta msaada wanapopitia matatizo haya japo kuna matibabu na masuluhisho mazuri sana ya matatizo hayo

Changamoto kubwa mbili

Kupungua kwa homoni ya testosterone

Kumeonekana kupungua kwa homoni ya testosterone kwa wanaume ukilinganisha na miaka mingi iliyopita ni wazi kwamba mazingira na mitindo ya kimaisha yanachangia tatizo hili zaidi hali hii inachochewa zaidi na mazingira ya kisasa tunayoishi hivi sasa na pia ongezeko la matatizo kama uzito mkubwa "obesity" kila kukicha tatizo hili linazidi kuongezeka

Matatizo ya nguvu za kiume

Mambo kama vile milo ya kisasa,ukosefu wa usingizi wa kutosha,msongo wa Mawazo,ongezeko la matatizo kama vile kisukari ,uvutaji wa sigara,matumizi makubwa ya pombe,matumizi ya aina Fulani za dawa

Kumekuwa na ongezeko la uzito mkubwa "obesity" na kisukari nayo pia yanaonekana kuongeza hatari zaidi ya matatizo haya

mtu mwenye uzito mkubwa ana hatari zaidi ya kujikuta katika matatizo haya ukilinganisha na yule mwenye uzito wa wastani

Ripoti za mwaka jana zinaonyesha kwamba watu wenye matatizo ya moyo wana hatari mara 3 zaidi ya kujikuta ana changamoto za nguvu za kiume

Sababu zingine ambazo huwa hazijadiliwi sana ni uchafuzi wa hewa ,na matumizi mabaya ya “steroids”

Tafiti zipo wazi kwamba matumizi makubwa ya homoni kama vile testerterone "steroids" yanaweza kuharibu uzalishwaji wa kawaida wa homoni hiyo mwilini jambo ambalo linaathiri zaidi uwezo wa mwili kuzalisha homoni hiyo kwa ufanisi “shuts down the natural production” Hii hasa inasukumwa zaidi na mitazamo ya wanaume wengi kutaka miili mikubwa kutunisha misuli,inachangia matumizi mabaya ya steroids na matumizi hayo yanachangia hormone imbalance na kuleta matatizo ya afya ya uzazi

Ongezeko la uchafuzi wa mazingira

“Chembe za plastiki zinaathiri ubora wa mbegu za kiume” kemikali kama vile BPA ambayo inatumika katika kutengeneza plastiki na inatumika katika vyombo vya chakula kama zina athari katika afya ya uzazi na kuoenekana kama jambo ambalo linachangia baadhi ya matatizo katika afya ya uzazi mojawapo ni kwamba zinaathiri ubora wa mbegu za kiume pia huweza kuvuruga utaratibu wa kawaida wa homoni mwilini mwa mtu ,hiyo ni moja wapo tu kati ya zile ambazo zinaitwa "endocrine disruptors" kemikali hizi zipo katika bidhaa nyingi tunazozitumia kila siku

Perfomamnce anxienty 

Inatokeaje?

Mtu anapokuwa na wasiwasi juu ya uwezo wake hasa katika swala zima la uzazi uoga huo husababisha yeye kushindwa kushiriki vyema katika tendo kwani anapokuwa na wasiwasi/uoga moja ya kitu kinatokea ni kwamba mwili baadhi ya homoni kama vile adrenaline zitaachiliwa na kwa namna moja ni kwamba zitasababisha kupungua kwa kiasi cha damu kinachokwenda katika sehemu kama vile uume na sehemu zingine hivyo anaweza akajikuta anapata tatizo la Erectile dysfunction na kibaya zaidi ni kwamba ikitokea mara moja hali hii na isipopata kutatuliwa (yaani mtu kuangalia namna ya kuondokana na uoaga/wasiwasi huo) kinachotokea ni kwamba hali hiyo itajirudia tena siku nyingine linakuwa tatizo la kudumu

inawapata sana vijana wadogo miaka 20+ kundi hili utakuta kimwili kila kitu kipo sawa ila uoga huu ndio unaowakwamisha

Tatizo hili linaongezeka kadiri ambavyo halishughulikiwi yaani mtu anapatwa na kile ambacho kinaitwa “snow ball effect” kwamba kadiri ambavyo mtu hajashughulika kutatua tatizo hili linapojitokeza mara ya kwanza litaendelea kumsumbua na mwisho wa siku atakuwa ana hofu ya kushiriki tendo “sexual avoidance”

Ielewe zaidi performance anxienty

Ni moja kati ya kitu ambacho kinachangia tatizo hili kwa asilimia kubwa hali hii inaweza ikasababisha wasiwasi mkubwa wa mtu kuelekea kufanya tendo na wakati mwingine lisiposhughulikiwa kwa haraka linaweza likasababisha hata uoga wa mtu kujihusisha katika tendo kabisa

Tuone nini wanaume wanaogopa zaidi wakiwa katika hali hii

·         Wanaogopa kusimamisha uume

·         Wanaogopa kwamba hawataweza kumridhisha mweza

·         Wanaogopa kwamba labda uume wake utaonekana ni mdogo ukilinganisha na aliyepita (x-partner)

·         Wanaogopa sana kuhusu “pre mature ejaculation”(kumwaga mapema)

Tafiti zinaonyesha kwamba linapokuja swala la performance anxienty wanaume wengi wenye hali hiyo huogopa mambo hayo hapo juu na mara nyingine inachangiwa na tabia kama vile kuangalia video za ngono mitandaoni wanaanza kuwa na wasiwasi wakilinganisha labda uume wake na aliouona katika video ,ama muda ambao walio katika video walitumia ataogopa je na mimi nitaweza Kwenda kwa muda wote huo? Je nitamfikisha kileleni? Yote hayo husababisha wasiwasi na huweza kupelekea mwanaume kushindwa kufanya vyema katika tendo

Hapa suluhisho kubwa ni mtu kutatua hali hiyo ya uoga ama msongo wa Mawazo bila hivyo tatizo hilo litaendelea kukua na kukua zaidi

Habari njema ni kwamba unaweza kuimarisha nguvu za kiume kwa kuzingatia mitindo mizuri ya kiafya ambayo yataelezwa zaidi hapa chapisho linalofuata litahusu suluhisho la tatizo hili unaweza ukasoma zaidi hapa kujua  kufanya (shuka hadi chini utaona sehemu pameantikwa "mens health" bonyeza chapisho limeandikwa Suluhisho 1"

au bonyeza hapa kusoma sehemu ya kwanza ya  Suluhisho

Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...