KWANINI MARA NYINGI JUHUDI ZA KUPUNGUZA UZITO HUISHIA NJIANI?
Mwili wa binadamu una uwezo wa kukinza kupungua uzito kutokana na mchanganyiko wa sababu za kisaikolojia, homoni, na mtindo wa maisha, na hivyo kufanya iwe changamoto kudumisha uzito mzuri. Mabadiliko mbalimbali katika usawa wa homoni, na hata utendaji wa mwili huchangia katika kuleta ukinzani
Michael Rosenbaum, Daktari na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, ambaye hufanya utafiti kuhusu jinsi miili yetu inavyopambana na kupunguza uzito, anasema,"We are richly endowed with genes that favor the storage of calories as fat." akimaanisha kwamba "Tumejaliwa sana na jeni zinazolinda uhifadhi wa kalori kama mafuta." Tabia ya kupata uzito na ugumu wa kuupunguza na kuuondoa haswa linachangiwa na mambo mengi na sio sana kuhusu swala la uvivu na ulafi. mara nyingi tunaweza tukaweka bidii ili kupungua uzito na juhudi zisipoleta matokeo sahihi huwa tunajilaumu kwamba ni uzembe au wadhaifu au hatuna bidii
Mwili Wako Unavyoshughulikia Kupunguza Uzito
Mlo na mazoezi kwa kawaida huchukuliwa kama njia kuu za kufikia uzito mzuri. Lakini, kwa nini wakati mwingine hatuoni matokeo tunayotarajia?
Suala ni kwamba mwili wako hauko tayari kuachilia uzito kwa urahisi. Una mifumo ya kujilinda iliyojengwa ndani ili kukuweka katika kiwango chako cha kawaida cha uzito. Unapojaribu kupunguza uzitowakati mwingine mwili hutoa homoni zaidi ya ghrelin"homoni ya njaa" ambayo huongeza hisia za njaa, na hupunguza uzalishaji wa homoni ya leptin, ambayo husaidia kuhisi kushiba. Hii ina maana kwamba njaa unayohisi wakati unapambana kupunguza uzito sio swala la kwamba huwezi kujizuia bali ni mabadiliko ya homoni ambayo hufanya iwe vigumu sana kushikamana na "diet" kwa muda mrefu. Njaa unayohisi sio ishara kwamba huna nguvu za kujizuia au mdhaifu . Ni mabadiliko ya homoni ambayo hufanya iwe ngumu sana kwako kushikamana na lishe yako kwa muda mrefu.
Sababu Zinazochangia Ugumu wa Kupunguza Uzito
Mbali na maelezo yaliyotajwa hapo juu, kuna sababu zingine kadhaa zinazoweza kufanya kupunguza uzito kuwa changamoto:
Mabadiliko ya Homoni:
Usawa mbaya wa homoni: viwango vya juu zaidi vya homoni kama vile insulini na homoni za stress huongeza zaidi ugumu wa kupungua uzito Lishe inaweza kuathiri viwango vya homoni kama leptin na ghrelin, ambazo huathiri hamu ya kula na juhudi za kupunguza uzito. soma zaidi utafiti kuhusu viwango vya juu vya insulin na ongezeko la uzito viwango vya juu vya insulin huchochea zaidi utunzwaji wa mafuta mwilini
Stress: Msongo sugu huongeza viwango vya cortisol, ambayo huongeza hamu ya kula, haswa kwa vyakula vyenye sukari na mafuta, na kukuza uhifadhi wa mafuta, haswa katika eneo la tumbo.
Umetaboli na Nadharia ya set point:
Uzito wa set point: Mwili unaweza kuwa na set point yaani kiwango fulani cha uzito cha juu kilichoathiriwa na vinasaba, ambacho siku zote hujaribu kudumisha,kupambana usishuke zaidi ya kiwango hiko na kufanya iwe vigumu kupunguza uzito na kuuondoa.
Mambo Mengine:
Ukinzani wa Insulini: Seli zinapokuwa sugu kwa insulini, gucose haiwezi kutumika kwa nishati na badala yake huhifadhiwa kama mafuta, na hivyo kufanya kupunguza uzito kuwa changamoto zaidi.
Usingizi na hali ya kiafya ya Utumbo "gut health": Ukosefu wa usingizi huvuruga homoni zinazodhibiti hamu ya kula, na afya duni ya utumbo "poor gut health" huathiri ufyonzaji wa virutubishi na metabolism
Hali ya kiafya ya mtu : Hali kama vile hypothyroidism na ugonjwa wa polycystic ovary (PCOS) zinaweza kuathiri uzito wa mtu
Mikakati ya kupambana na ugumu wa kupunguza uzito
Ingawa kupunguza uzito kunaweza kuwa changamoto, kuna mikakati kadhaa ambayo inaweza kusaidia:
Lishe: Ingawa lishe pekee haifanyi kazi, kula vyakula vyenye lishe kama vile protini matunda, na mboga ni muhimu.
Mazoezi: Mazoezi ni muhimu sana. Sio tu kwamba huchoma kalori, lakini pia husaidia kuhifadhi na kuongeza misuli ambayo husaidia uchomaji wa kalori kwa ufanisi zaidi hata muda ambao hufanyi mazoezi kwa kuwa misuli huchoma kalori haraka kuliko mafuta, hii husaidia kubadilisha kiwango chako cha kawaida cha uzito misuli pia husaidia ufanyaji kazi mzuri wa homoni ya insulin na pia husaidia kuweka sawa homoni zako Mazoezi ya nguvu kama vile kuinua uzito Kumbuka kuwa BMI yako inaweza isipungue au hata kuongezeka kidogo unapoongeza misuli, lakini kubadilisha muundo wa mwili wako kuwa na misuli zaidi ni mafanikio, hata kama uzito wako unabaki sawa.
Usingizi: Hii ni muhimu sana tafiti zinaonyesha kwamba usiku mmoja tu wa kukosa uzingizi "sleep deprivation" huongeza homoni za njaa mara nyingi zaidi siku inayofuata hivyo utajikuta unakula sana soma matokeo ya utafiti huo hapa angalia matokeo ya utafiti huo hapa kupata usingizi wa kutosha ni muhimu kwa udhibiti wa homoni. Ukosefu wa usingizi unahusishwa na kuongezeka kwa homoni za njaa na kupungua kwa homoni za "kushiba" yaani "leptin"hivyo unapokuwa katika harakati za kupunguza uzito jitahidi kupata usingizi wa kutosha
Udhibiti wa Msongo: Kuishi na kiwango cha juu cha msongo huathiri homoni zinazodhibiti hamu ya kula. Kudhibiti msongo kupitia mbinu kama vile kutafakari, kupumua kwa kina, na yoga kunaweza kusaidia kupunguza kiwango chako cha kawaida cha uzito na kuboresha ubora wa maisha yako.

Join the conversation