Hormone balance:Elewa kuhusu homoni zako
ELEWA KUHUSU HORMONE BALANCE
Homone balance ni nini? Ni hali ya kuwepo na usawa katika uzalishwaji na utendaji kazi wa homone mwilini ni tunaishi katika kipndi ambacho swala la homone balance halitokei tu unahitaji kuelewa na kujiwekea mikaka kwani tunaishi katika mazingira ambayo yanavuruga usawa wa homoni na wakati mwingine unafanya mambo ambayo yanaweza yakaathiri "hormone balance"yako
kipengele cha kisaikolojia
Tunapopitia msongo wa Mawazo/upweke kutokana na mikazo na presha mbalimbali za maisha,mahusiano na kazi miili yetu huachilia homoni ya stress kitaalamu inaitwa “cortisol” hali ikiendelea hivyo hivyo kwa muda mrefu madhara huanza kuonekana mwilini mwa mtu kwani viwango vya juu vya homoni hii inaweza kuleta mvurugiko wa homoni zingine muhimu mwilini hivyo huathiri usingizi,kinga ya mwili,hali ya kihisia “mood” ,mvurugiko wa hedhi ,kupungua kwa homoni nyingine za muhimu kama vile “testosterone”
Kipengele cha uzito
Uzito wa mtu “body weight” una mchango pia katika kuamua ufanyaji kazi wa homoni unaweza ukaathiri mfumo wa homoni
Mfano kwa wanaume wenye viwango vingi vya mafuta mwilini seli za mafuta “fat cells” huachilia kemikali iitwayo “aromatase” ambayo huibadili homoni iitwayo testosterone mara nyingi hujulikana kama homoni ya kiume Kwenda kuwa aina Fulani ya estrogen ambayo hujulikana sana kama homoni ya kike hivyo basi viwango vikubwa vya mafuta hupelekea kutokuwa na usawa katika homoni mwilini mwa mtu huyo
Kipengele cha urithi/genetics
“Genes run in the family -jeni zinatembea kwenye familia"
Genetics/jenitiki huamua namna gani baadhi ya homoni zinavyofanya kazi hivyo kunaweza kuwa na utofauti kati ya mtu mmoja na mwingine kulingana na jenetiki kutokana na hali ya urithi
Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba jenetiki peke yake haiwezi kujitosheleza kama kipengele kinachoathiri mfumo wa homoni vipo vipengele vingine tutakavyoviona hapo mbele
Ndio maana tunasema "genes load a gun but enviroment and lifestyle pulls the trigger" jenetiki zinamuweka mtu katika hatari kwanza lakini sio lazima kwamba tatizo hilo lionekane kwa mtu huyo tatizo litaonekana zaidi pale ambapo mazingira na mitindo ya kimaisha ya mtu yatachichea zaidi tatizo ambalo lilikuwa kimya mwanzo
Magonjwa sugu
Uwepo wa magonjwa sugu kama vile kisukari aina ya pili japo ugonjwa huu nao unatokana na katika ufanyaji kazi wa homoni ya insulin unaweza kuja na matatizo mengine makubwa zaidi katika mfumo wa homoni Ukinzani wa insulini huleta athari katika homoni nyingine
kuelewa zaidi kuhusu ukinzani wa insulini bonyeza hapa elewa kuhusu ukinzani wa insulini "
kwa mfano kwa wanawake ukinzani wa insulini huchangia matatizo ya polycystic ovary syndrome (PCOS) tatizo ambalo linasemekana kuwa ni chanzo kikubwa cha "utasa" "infertility" kwa wanawake, ambapo kunakuwa na mvurugiko katika homoni kama vile estrogen
kwa upande wa wanaume unaweza ukapelekea viwango vya chini vya homoni ya "testersterone" hapo utaona dalili kama vile kukosa hamu ya tendo "low libido" na zingine
Sababu za Mazingira
Kemikali zinazovuruga mfumo wa homoni kitaalamu huitwa "endocrine disruprors" Kuathiriwa na kemikali fulani zinazopatikana katika plastiki, dawa za kuua wadudu, na bidhaa zingine zinaweza kuingia mwilini na kuleta mvurugiko katika utendaji kazi wa kawaida wa mfumo wako wa homoni
Ni muhimu kuelewa kwamba mfumo wa homoni unaweza kuathiriwa na hata viwango vya chini vya kemikali hizi vinaweza kuwa na athari kubwa."
Umri na maendeleo
Mfumo wako wa homoni hubadilika kutokana na hatua mbalimbali za maisha yako na umri pia
hatua mbalimbali za maisha
Balehe:mabadiliko makubwa ya homoni hutokea wakati wa balehe
Ujauzito:Viwango vya homoni hubadilika sana wakati wa ujauzito hivyo kuna mabadiliko pia katika mwili yataonekana
Kukoma kwa hedhi "menopause":wanawake hupitia kipindi cha kupungua viwango vya estrojeni wakati wa kukoma kwa hedhi
Uzee:Viwango vya homoni hubadilika kadiri tunavyokua mfano uzalishwaji wa homoni ya kiume "testesterone" kwa mwanaume wa miaka 70 ni tofafauti na kijana mwenye miaka 20
Mtindo wa maisha:
Lishe:Lishe duni hasa vyakula vilivyosindikwa sana "highly processed foods" ,vyakula vyenye sukari nyingi yanaweza yakaathiri uzalishwaji na utendaji kazi wa homoni mbalimbali mwilini
Usingizi:usingizi wa kutosha ni muhimu sana katika udhibiti wa homoni kama umekuwa ukichukulia poa usingizi bonyeza hapa Usingizi na hormone balance
kuelewa zaidi usingizi unavyoathiri homoni mwilini mwako
Mazoezi :mazoezi yanachangia sana ufanyaji kazi na uzalishwaji wa homoni mwilini mwako mfano kwa wanawake viwango vya juu vya homoni ya estrogen huongeza hatari zaidi ya saratani lakini mazoezi yameonekana kuwa na faida katika kupunguza hatari hiyo na kwa upande wa wanaume mazoezi yanasaidia kuweka sawa na kuongeza viwango vya homoni ya testesterone bonyeza hapa kuelewa zaidi kuhusu mazoezi na homoni Mazoezi na hormone balance
Yapo mambo unaweza kuyafanya kuanzia leo ili kuweka sawa mfumo wako wa homoni dhibiti msongo wa mawazo,zingatia vyakula bora,zingatia mazoezi,pata usingizi wa kutosha
"Elewa kisha tekeleza kwaajili ya afya yako na uwapendao"
Ijali afya yako

Join the conversation