Mazoezi na GABA :Siri ya kupambana na changamoto za afya ya akili

 



Baada ya kuonekana na dalili karibu zote za depression Nina anaamua kwenda hospitali na huko anaonekana kuwa na tatizo la depression na kutokana kwamba tatizo lilifikia kiwango cha kuyasumbua maisha yake ya kawaida ,kazini maendeleo yake hayakuwa mazuri ,mwili wake ulidhoofika wakati huo alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara na tokea hapo alianza kufanya mazoezi 

Nina anasema "Kama kukimbia kumenifundisha kitu ni hiki mambo yanabadilika" aliandika katika kitabu chake cha Depression hates a moving target  (unaweza ukaisoma hapo)

Aliona namna ambavyo hali yake ilizidi kuimarika na hata kiwango cha dozi alichokuwa anakitumia kilizidi kupungua

Mazoezi yana siri gani na yanawezaje kutusaidia kupambana na janga la matatizo ya afya ya akili ambayo yanaongezeka kila kukicha?

Mazoezi,yameonyesha kuongeza uzalishwaji wa GABA kwenye ubongo.Ongezeko hili la GABA linasaidia  kuchangia faida za mazoezi kwenye kuweka sawa hisia, wasiwasi, na ustawi wa jumla wa akili.

GABA ni nini?

Ni moja kati ya  kemikali inayozalishwa katika ubongo tofauti yake na kemikali zingine ni kwamba wakati zingine zinachangamsha seli za ubongo na kutuma signals zaidi GABA yenyewe inafanya kazi ya kutuliza na signal kufanya zizalishwe taratibu zaidi hivyo kuleta utulivu,na afya njema ya akili 

GABA na Mazoezi

Mazoezi makali, hasa yanapofanywa kwa kati ya dakika 8-20, yanaweza kusababisha kuongezeka kwa uzalishaji na utoaji wa GABA kwenye ubongo.

Faida

Viwango vilivyoongezeka vya GABA baada ya mazoezi vimehusishwa na kuboresha hisia, kupunguza wasiwasi, na kusaidia ufanyaji kazi wa ubongo (yaani cognitive function)

GABA na Kusoma

Tafiti zinaonyesha kuwa mazoezi yanaweza kuboresha utendaji kazi wa GABA hivyo huimarisha usomaji ,uchangamfu na uwezo wa kuzingatia (focus) 

Je unaweza kuipata GABA kwenye chakula ?

Huenda ungependa kujua ni chakula gani au kitu gani labda unaweza kukitumia kama chanzo cha GABA ukweli ni kwamba ,GABA haipatikani kwa urahisi kwenye vyakula vingi ila kuzingatia mlo mzuri husaidia katika uzalishwaji wake mwilini 

Umeona ni kwa namna gani kwa kiwango kikubwa mazoezi yanasaidia uzalishwaji zaidi wa GABA na faida zake kwa afya ya akili hivyo unaweza ukajipanga kuanza kufanya mazoezi kwaajili ya afya yako ya akili

Tafiti za kurejea:Rejea tafiti hii hapa chini kuona uhusiano wa GABA na mazoezi

 https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC11457286/

Ukiachilia mbali changamoto za afya ya afya kama vile wasiwasi "anxienty" na depression tatizo la ADHD linazidi kuongezeka ila mazoezi pia yana mchango mkubwa katika kupambana na tatizo hilo

Mazoezi yalivyomsaidia kupambana na ADHD


Health Talks... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...